Ezekiel 32:11-13

11 a“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Upanga wa mfalme wa Babeli
utakuja dhidi yako.
12 bNitafanya makundi yako ya wajeuri kuanguka
kwa panga za watu mashujaa,
taifa katili kuliko mataifa yote.
Watakivunjavunja kiburi cha Misri,
nayo makundi yake yote
ya wajeuri yatashindwa.
13 cNitaangamiza mifugo yake yote
wanaojilisha kando ya maji mengi,
hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu
wala kwato za mnyama
hazitayachafua tena.
Copyright information for SwhNEN